• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    IBRAHIMOVIC AFUNGA BAO LA 51 SWEDEN IKITOA SARE YA 1-1 NA MONTENEGRO KUFUZU EURO 2016

    BAO la dakika za mwishoni la Stevan Jovetic kwa penalti usiku wa kuamkia leo limeipa Montenegro sare ya 1-1 na Sweden katika mchezo wa Kundi G kufuzu Euro 2016 baada ya Zlatan Ibrahimovic kuwafungia wageni bao la kuongoza kipindi cha kwanza.
    Hilo linakuwa bao la 51 kwa Ibrahimovic anayeshikilia tuzo ya Bao Bora la Mwaka duniani tangu aanze kuichezea timu yake ya taifa, Sweden. 
    Matokeo hayo yanaiacha Sweden nafasi ya pili katika kundi hilo, ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi nne, moja mbele ya Montenegro na Urusi na nne nyuma ya vinara, Austria waliofunga Urusi 1-0 mapema jana kubaki kileleni.
    Sweden walijisikia vibaya baada ya refa Mscotland, William Collum kukataa bao la dakika za nyongeza la kiungo, Albin Ekdal, ambalo lngewapa ushindi.
    Zlatan Ibrahimovic is congratulated by his Sweden team-mates after scoring in the ninth minute
    Zlatan Ibrahimovic akipongezwa na wachezaji wenzake wa Sweden baada ya kufunga dakika ya tisa
    Ibrahimovic controls the ball as Montenegro's Zarko Tomasevic attempts to close him down 
    Ibrahimovic akimiliki mpira mbele ya beki wa Montenegro, Zarko Tomasevic 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2836182/Zlatan-Ibrahimovic-s-51st-international-goal-cancelled-late-Stevan-Jovetic-penalty.html#ixzz3JCp82oSC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IBRAHIMOVIC AFUNGA BAO LA 51 SWEDEN IKITOA SARE YA 1-1 NA MONTENEGRO KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top